LONDON : Maelfu waandamana kupinga vita | Habari za Ulimwengu | DW | 25.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Maelfu waandamana kupinga vita

Maelfu ya waandamanaji wanaopinga vita wamekusanyika katikati ya London kutowa wito wa kuondolewa kwa wanajeshi wa Uingereza kutoka Iraq.

Maandamano hayo ni makubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa kwa miaka kadhaa nchini humo.Waandamanaji wakibeba mabango walifurika kwenye uwanja wa Trafalgar katika maandamano hayo yaliowashirikisha wanasiasa,wana burudani na familia za wanajeshi 132 wa Uingereza waliouwawa nchini Iraq tokea kuvamiwa kwa nchi hiyo hapo mwaka 2003.

Hapo Jumaatano Waziri Mkuu Tony Blair ametangaza kwamba idadi ya wanajeshi wa Uingereza walioko Iraq itapunguzwa kwa wanajeshi 1,600 hadi 5,000 katika miezi michache ijayo na upunguzaji zaidi yumkini ukafanyika baadae mwaka huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com