LONDON : Hasina azuwiwa kurudi Bangladesh | Habari za Ulimwengu | DW | 23.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Hasina azuwiwa kurudi Bangladesh

Waziri Mkuu wa zamani wa Bangladesh Sheikh Hasina Wajed amezuiliwa kupanda ndege iliokuwa ikielekea Dhaka mji mkuu wa Bangladesh kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Heathrow mjini London hapo jana baada ya serikali ya Bangladesh kuyataka mashirika ya ndege kumzuwiya mama huyo asirudi nyumbani Bangladesh.

Shirika la ndege la Uingereza British Airways limemwambia Hasina kwamba ndege yake isingeliweza kuingia Bangladesh yeye akiwemo kwenye safari hiyo.

Mapema mahkama ya Dhaka ilitowa hati ya kukamatwa kwa Hasina kiongozi wa chama cha Awami Leagur kwa madai ya mauaji ya watu wanne wakati wa ghasia mjini Dhaka mwezi wa Oktoba mwaka jana.

Hatua hiyo inakuja wakati kukiwa na harakati za kupiga vita rushwa za serikali ya mpito inayoungwa mkono na jeshi.

Serikali inasema inataka kuusafisha mfumo wa kisiasa kwa kuwalizimisha Hasina na mpinzani wake mkuu Khaled Zia kuishi uhamishoni baada ya kuzidhibiti siasa za Bangladesh kwa miaka 15.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com