1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Blair amehojiwa kuhusu michango ya vyama

Polisi nchini Uingereza kwa mara ya pili wamemuhoji waziri mkuu Tony Blair katika uchunguzi unaofanywa kuhusu michango ya pesa inayokusanywa na vyama vya kisiasa.Msemaji wa waziri mkuu aliwaambia waandishi wa habari kuwa Blair alihojiwa kama shahidi,katika ofisi yake ya Downing Street,Ijumaa iliyopita.Tony Blair alihojiwa mara ya kwanza Desemba mwaka jana. Polisi wanachunguza ikiwa chama cha Labour na vyama vingine pia viliahidi kuwapa wafuasi wake vyeo katika Baraza la Malodi,badala ya mikopo ipatayo mamilioni ya Pauni za Kingereza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com