1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Azma ni kuwakabidhi Wairaki mamlaka ya usalama

4 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSp

Waziri Mkuu wa Uingereza,Gordon Brown ametetea hatua ya kuondosha vikosi vya Uingereza kutoka makao yake makuu ya Basra nchini Irak.Amesema, lengo la hatua hiyo ni kuwakabidhi Wairaki mamlaka ya usalama upesi iwezekanavyo.Akaeleza kuwa majeshi ya Uingereza yatakayobakia kiasi ya kilomita 25 kutoka mji wa Basra,yanaweza kutumiwa ikiwa kutakuwepo haja hiyo.