LONDON : Ashtakiwa kwa mauaji ya makahaba | Habari za Ulimwengu | DW | 22.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Ashtakiwa kwa mauaji ya makahaba

Katika kesi ya mauaji ya makahaba watano katika mji wa mashariki wa Uingereza wa Ipswich polisi ya Uingereza imemfungulia mashtaka mwanaume mmoja kwa kuhusika na mauaji hayo.

Steven Wright mwenye umri wa miaka 48 dereva wa gari la mizigo anatuhumiwa kuwaua makahaba hao wote watano katika kipindi cha wiki chache na kuitia hofu Uingereza nzima kutokana na mauaji hayo kutokea kwa kipindi cha muda mfupi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya hivi karibuni nchini Uingereza.

Mtu wa pili mwenye umri wa miaka 37 ambaye pia alikamatwa wiki hii kwa tuhuma za mauaji hayo ameachiliwa kwa dhamana bila ya kufunguliwa mashtaka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com