1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : 100 wajeruhiwa baada ya treni kuacha njia

Takriban watu 100 wamejeruhiwa baada ya treni kuacha njia na kuteleza hadi chini kwenye tuta kaskazini mwa Uingereza.

Waokoaji wamesema baadhi ya abiria bado ingali wamekwama katika mojawapao ya mabehewa ya treni hiyo ambayo ilikuwa ikisafiri kutoka London kuelekea Glasgow huko Scotland. Taarifa za vyombo vya habari zimesema kwamba mtu mmoja ameuwawa na wengine saba hali zao ni mbaya ingawa maisha yao hayako hatarini.

Haijulikani nini kilichosababisha ajali hiyo.

Imeripotiwa kwamba kulikuwa na abiria 180 ndani ya treni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya reli ya Virgin ambayo ilikuwa ikisafiri kwa mwendo wa kilomita 150 kwa saa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com