LOME: Chama tawala Togo kimeshinda uchaguzi
19 Oktoba 2007Matangazo
Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi uliofanywa siku ya Jumapili nchini Togo,yaonyesha kuwa chama tawala RPT cha rais Faure Gnassingbe kimepata ushindi.Kwa mujibu wa ripoti ya Halmashauri ya Uchaguzi ya Taifa,chama cha RPT kimeshinda viti 49 katika bunge la viti 81.Chama cha upinzani UFC cha kiongozi alie uhamishoni,Gilchrist Olympio, kimepata viti 21.
Katika mwaka 2005,jeshi lilimpa madaraka Gnassingbe kufuatia kifo cha baba yake,Gnassingbe Eyadema alietawala nchini Togo kwa miaka 38.