LOME : Chama tawala chashinda uchaguzi wa bunge | Habari za Ulimwengu | DW | 18.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LOME : Chama tawala chashinda uchaguzi wa bunge

Chama tawala nchini Togo cha Rally of the Togolese People kimeshinda wingi wa viti bungeni kwa kujizolea viti 49 kati ya 81 katika uchaguzi wa bunge wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Jumapili chama cha upinzani cha UFC kimepata viti 21 na chama cha CAR kimepata viti vitano.Matokeo ya viti saba vilivyobakia yanaendelea kuhesabiwa na yanatazamiwa kutolewa baadae leo hii.

Asilimia 95 ya watu wamejitokeza kupiga kura ambapo vyama vya upinzani vilishiriki kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 13.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com