Loew aonya kuhusu kuwachosha wachezaji
1 Juni 2017"Ni mchezo hatari , hatupaswi kuvuta kamba kwa nguvu sana," kocha mkuu wa Ujerumani alionya katika mahojiano yaliyofanyika leo Alhamis na SID, tawi la shirika la habari la Ufaransa AFP.
"Unakuwa na hisia kwamba vitu tayari vimepauka na orodha ya timu zinazocheza inaonekana kuwa ya furaha."
loew amewaacha wachezaji nyota katika kikosi chake kama Thomas Mueller , Mats Hummels, Toni Kroos, Mesut Ozil , Jerome Boateng , Manuel Neuer na sami Kherdira kwa ajili ya michuano hiyo ya Confederation Cup, inayoanza Juni 17 na kumalizikia Julai 2, na amewaita wachezaji wapya kabisa saba.
Kujitayarisha kwa ajili ya kombe la dunia mwakani, Loew amesema lengo lake kuu nchini Urusi ni kutia damu changa katika kizazi cha wachezaji wake nyota , na hakusema lolote kuhusu kushinda katika mpambano huo wa timu nane.
Ujerumani inakutana na Chile , Australia na Cameroon katika kundi B wakati Ureno , inakumbana na wenyeji Urusi , Mexico na New Zealand katika kundi A.
Loew amewajumuisha wachezaji watatu tu wa kikosi cha kwanza ambacho kilishinda kombe la dunia mwaka 2014 na bila kuwa na walinzi watatu Matthias Ginter, Shkodran Mustafi na mchezaji wa kati Julian Draxler , ambao walikuwamo katika kikosi cha kwanza katika fainali ya mjini Rio de Janeiro.
Akiweza kuifikisha timu ya Ujerumani katika awamu ya nusu fainali ya kila michuano mikubwa ya fainali tangu mwaka 2006, Loew anaonya kwamba mipango ya FIFA na UEFA kupanua mashindano makubwa kunaweza kusababisha mzigo mkubwa kwa wachezaji na vilabu.
Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe