1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LISBON:Umoja wa Ulaya kuwa mstari wa mbele katika masuala ya ulimwengu

19 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7EQ

Viongozi wa Umoja wa Ulaya hii leo wameendelea na majadiliano kuhusu namna ya kuwa mstari wa mbele katika masuala ya ulimwengu mfano mabadiliko ya hali ya anga pamoja na misukosuko katika soko la hisa ulimwenguni.Makubaliano mapya ya kufanya mageuzi katika Umoja huo hususan katiba yanawezesha mataifa 27 wanachama kuwa na nafasi muhimu katika masuala ya ulimwengu.Makubaliano hayo yaliyofikiwa baada ya saa sita jana usiku baada ya majadiliano yaliyodumu muda mrefu yanawezesha bara la Ulaya kujumuika kwa karibu zaidi na ushawishi mkubwa katika masuala ya sera za kigeni.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya Jose Socrates ambaye ni Waziri Mkuu wa Ureno,makubaliano hayo yatatiwa saini mjini Lisbon ifikapo Disemba 13.

''Safari hii hakukuwa na visababu na sababu za kuwafanya viongozi wa mataifa na serikali kutoafikiana.Ni mafanikio makubwa.Tunaweza katika dakika ya mwisho kutafuta suluhu ya baadhi ya mambo ambayo bado yanatatiza tukiwa na mtizamo wa pamoja wa Ulaya''

Azimio hilo jipya linapunguza idadi ya wabunge wa bunge la Ulaya vilevile maamuzi yatakayohitaji kuungwa mkono na mataifa wote wanachama badala yake wingi wa kura pekee ndio utakaotumika .Hata hivyo bendera ya pamoja na wimbo wa taifa havikubaliwi katika maafikiano hayo mapya.