LISBON: Pendekezo la kuregeza sheria ya kutoa mimba
11 Februari 2007Matangazo
Kura ya maoni inapigwa nchini Ureno hii leo,juu ya sheria kali za nchi hiyo kuhusika na kitendo cha kutoa mimba.Kura hiyo inahusika na pendekezo la serikali ya Ureno kuwa wanawake waruhusiwe kutoa mimba mpaka wiki 10 za mwanzo tu.Kwa hivi sasa,nchini humo wanawake wanaruhusiwa kutoa mimba ikiwa tu walibakwa,afya ya mzazi ipo hatarini au kama mimba changa ina kasoro fulani.