1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LISBON : Bemba kurudi nyumbani Septemba

Makamo wa rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Jean-Pierre Bemba ambaye hivi sasa yuko nchini Ureno anataka kurudi nyumbani kabla ya kuanza kwa kikao cha kwanza cha bunge hapo tarehe 15 mwezi wa Septemba.

Bemba amekaririwa akisema leo hii kwamba anatumai kurudi ifikapo tarehe 15 mwezi wa Septemba ili kutimiza wajibu wake wa kikazi.

Ameongeza kusema kwamba angelipenda kurudi nchini humo katika usalama kamili kwa kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa,Umoja wa Ulaya na anataraji pia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Bemba mwenye umri wa miaka 44 amekwenda Ureno rasmi kwa ajili ya matibabu ya mguu na baraza la senate bunge lilimpa ruhusa ya kuondoka nchini humo siku 60 kwa sababu za matibabu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com