LIBREVILLE:Rais Sarkozy akamilisha ziara yake Afrika
27 Julai 2007Matangazo
Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy yuko nchini Gabon akiwa katika mkondo wake wa mwisho wa ziara yake ndogo ya eneo la kusini mwa jangwa la Sahara.Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano kati ya Ufaransa na bara la Afrika.Rais Sarkozy alilakiwa na mwenyeji wake Rais Omar Bongo Ondimba ambaye amekuwa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika wa miaka 40.
Kiongozi huyo wa Ufaransa alitokea nchini Senegal ambako alitoa wito kwa bara la Afrika kuganga yajayo na kupanga mikakati ya uongozi bora.
Marais Nikolas Sarkozy na Omar Bongo wanafanya mazungumzo ya mwisho kabla kuzuru misitu ambayo ni vyanozo vya mvua aidha kukutana na makundi yasiyo ya kiserikali yanayoshughulika na mazingira.