1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libnan yatakiwa imchague rais wa maridhiano

Oummilkheir6 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cl1V

Cairo:

Jumuia ya nchi za kiarabu,imezitolea mwito pande zinazohasimiana nchini Libnan zimteuwe hatimae mgombea wa maridhiano Michel Suleiman kua rais wa nchi hiyo.Taarifa ya mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa jumuia ya nchi za kiarabu waliokutana mjini Cairo –Misri imesema Syria pia inaunga mkono mwito huo.Taarifa hiyo imezitaka pia pande zinazohasimiana zikubali kuunda serikali ya umoja wa taifa.Libnan inajikuta bila ya rais tangu November mwaka jana,baada ya mhula wa rais Emile Lahoud kumalizika.Baada ya mvutano wa muda mrefu, vyama vinavyounda serikali-vinavyoungwa mkono na nchi za magharibi na vile vya upinzani vinavyoelemea upande wa Syria vilikubaliana kumteuwa jenerali Michel Suleiman agombee wadhifa wa rais.Mzozo mwengine umeripuka hivi sasa kuhusiana na kufanyiwa marekebisho katiba.Bunge la Libnan linatazamiwa kukutana tena january 12 ijayo.