1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Learning by Ear - Uhariri wa magazeti

3 Juni 2011

Sio tu wasikilizaji wa vipindi vyetu vya Noa Bongo wanaotoa maoni yao kuvisifu. Pia vyombo vya habari vinazungumzia vipindi vyetu. Soma hapa kuhusu yanayosemwa na vyombo hivyo.

https://p.dw.com/p/RRdT

"Tunapenda hadithi na hupendelea sana kuzisikiliza. Hivyo ndivyo iilivyokuwa kama desturi ya bara hili – kuelezea hadithi kwa kusimulia ina maana kubwa barani Afrika kuliko sehemu nyingine za ulimwengu," alidokeza msanii mmoja muigizaji aliyeshiriki katika utayarishaji wa vipindi nchini Msumbiji. Ni dhahiri kwamba vyombo vya habari ambavyo kwa asilimia 50 vko huru, hasa redio - inaweza kuchangia kuwaelimisha na kuwahamasisha Waafrika. Michezo ya redio imeanza kupata umaarufu na kutoa ushindani kwa utangazaji wa kawaida wa habari kote ulimwenguni. Kama vimetayaishwa vizuri, huwapa vijana mawazo mazuri. Kupitia njia hii, michezo ya redio ya Deutsche Welle vinakaribiana sana na hali halisi ya maisha ya kila siku"

(Süddeutsche Zeitung)

"Vipindi vya dakika kumi vinawalenga vijana hasa wa kati ya umri wa miaka 12 hadi 20, na wengi wa vijana wanaosikiliza vipindi hivi nchini Msumbiji ni wa umri wa hadi miaka 20. Kutokana na msukumo wa ufanisi wa michezo ya kuigiza kwenye televisheni kote ulimwenguni na ufadhili wa wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Ujerumani, michezo hiyo imezingatia mada kama vile uharibifu wa misitu, uhifadhi wa mazingira, ugonjwa wa malaria na ukimwi. Takriban nusu ya idadi ya wakaazi nchini Msumbiji hawajui kusoma na kuandika na redio ni chombo muhimu cha mawasiliano," alieleza msanii Vaz."

(Die Welt)

"Vijana wamechoshwa na mihadhara ya kila mara kuhusu mada kama vile ugonjwa wa ukiwmi na magonjwa mengine. Lakini ujumbe huu unapotolewa kwa mfano wa hadithi kupitia michezo ya kuigiza, basi vijana hao huwa na hamu kubwa ya kufuatilia michezo hiyo na ujumbe unapokelewa vizuri zaidi. Kuna sababu kwa nini michezo hii ya redio inatayarishwa barani Afrika. Mbali na Msumbiji michezo hii hutayarishwa Rwanda na pia Senegal.

Sababu kubwa ni kudumisha sura ya Afrika katika utayarishaji wake, ili viweze kukubalika kwa urahisi miongoni mwa wasilikizaji wetu kama kitu kilichotayarishiwa nyumbani. Wengi wa waandishi na wasimulizi wa michezo hii wanatoka barani Afrika."

(Frankfurter Allgemeine Zeitung)