Laurent Gbagbo akataa kung'atuka madarakani
4 Januari 2011Matangazo
Leo,viongozi hao watakutana na Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alie pia mwenyekiti wa hivi sasa wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Magharibi ECOWAS.
Marais wa Benin,Sierra Leone na Cape Verde wakiwakilisha ECOWAS na Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga kwa niaba ya Umoja wa Afrika walikwenda Cote d'Ivoire ambako walikuwa na mazungumzo pamoja na Gbagbo kabla ya kuonana na Ouattara.
ECOWAS imetishia kutumia nguvu za kijeshi ikiwa Gbagbo atakataa kumkabidhi madaraka Ouattara anaetambuliwa na jumuiya ya kimataifa kuwa ni mshindi wa uchaguzi uliofanyika mwezi wa Novemba.Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari,Gbagbo ameahidiwa na viongozi hao wa Kiafrika usalama wake na kwamba hatoshtakiwa ikiwa ataondoka kwa amani.