1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LARNACA: Steinmeier ametembelea vikosi vya wanamaji wa Kijerumani

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amevitembelea vikosi vya wanamaji wa Kijerumani katika manowari yao kwenye mwambao wa kisiwa cha Cyprus.Vikosi hivyo ni sehemu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa na vinalinda njia ya bahari,kwenye pwani ya Lebanon kwa azma ya kuzuia usafirishaji wa silaha za magendo kwa chama cha Hezbollah nchini Lebanon.Hapo awali,Steinmeier alipokuwepo mji mkuu wa Lebanon,Beirut,alitoa mwito kwa serikali za kigeni kutoingilia mambo ya ndani ya Lebanon.Mjini Beirut,waandamanaji wa Hezbollah na wafuasi wake wanaoiunga mkono Syria, wanamshinikiza waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora ajiuzulu.Waziri Steinmeier leo jioni anakwenda Israel.Ziara yake ya siku nne katika Mashariki ya Kati imepangwa kukamilishwa nchini Syria.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com