LAGOS:wazazi wa wabunge wawili watekwa nyara | Habari za Ulimwengu | DW | 13.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LAGOS:wazazi wa wabunge wawili watekwa nyara

Watu waliojihami kwa bunduki wamemteka nyara mama wa mbunge mwingine katika jimbo la kusini la Bayelsa nchini Nigeria baada ya kumteka nyara baba yake mbunge mmoja hapo awali.

Polisi wamefahamisha kwamba mama yake mbunge Delight Igali alitekwa nyara kutoka nyumbani kwake katika kijiji cha kusini cha Ijaw.

Kisa hicho kimefuatia kutekwa nyara baba yake mbunge Edowe Komonibo. Mzee huyo mwenye umri wa miaka 82 alaitekwa nyara kutoka nyumbani kwake.

Polisi pia wamefahamisha kuwa baba yake naibu spika wa bunge wa jimbo jirani la River State Charles Befii Nwile pia alitekwa nyara.

Taarifa ya polisi imesema kuwa wametia mbaroni mshukiwa mmoja ambae anahojiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com