LAGOS:Obasanjo arudi Chuo Kikuu | Habari za Ulimwengu | DW | 08.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LAGOS:Obasanjo arudi Chuo Kikuu

Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo amerejea chuo kikuu ikiwa ni majuma mawili tangu kuondoka madarakani.Kiongozi huyo wa zamani aliye na umri wa miaka 70 ameanza masomo katika Chuo Kikuu cha Open University kilichoko mjini Lagos.Bwana Obasanjo alikuwa madarakani kwa mihula miwili ya miaka minane iliyomalizika mwezi Mei tarehe 29 mwaka huu.

Bwana Obasanjo aliyejisajili kusomea masomo ya dini ya kikristo anahudhuria masomo mjini Abeokuta ulio katika jimbo la kusini magharibi la Ogun aliko na makao yake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com