LAGOS:Makamu wa Rais sasa ruhsa kugombea urais | Habari za Ulimwengu | DW | 08.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LAGOS:Makamu wa Rais sasa ruhsa kugombea urais

Mahakama kuu ya Nigeria imemuondolea kikwazo Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Atiku Aboubakary, cha kushiriki katika uchaguzi wa urais mwezi ujayo.

Tume ya uchaguzi ya Nigeria ilimuwekea kikwazo Atiku kuingia katika uchaguzi huo, baada ya kutajwa kuhusika na rushwa.

Jaji Babs Kuewumi wa mahakama kuu ya shirikisho la Nigeria,katika hukumu yake hapo jana alisema kuwa ni mahakama tu ndiyo yenye mamlaka ya kumuengua mtu kisheria kushiriki katika uchaguzi.

Atiku alijiengua kutoka katika chama tawala cha PDP kinachoongozwa na Rais Olesegun Obasanjo, baada ya kushutumiana hadharani na Rais Obasanjo, na anasimama katika uchaguzi huo kwa tiketi ya chama cha upinzani cha Action Congress.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com