LAGOS:Mahakama ya Rufaa nchini Nigeria yatupilia mbali rufaa ya Makamu wa Rais | Habari za Ulimwengu | DW | 03.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LAGOS:Mahakama ya Rufaa nchini Nigeria yatupilia mbali rufaa ya Makamu wa Rais

Mahakama kuu ya Rufaa nchini Nigeria leo imetupilia mbali rufaa ya Makamu wa Rais wa nchi hiyo Atiku Abubakar kupinga maamuzi ya tume ya uchaguzi kumzuia kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi ujayo.

Mapema mahakama ya rufaa ya Abuja alifutilia mbali uamuzi huo wa tume ya uchaguzi ya Nigeria, ikisema kuwa tume hiyo haina mamlaka ya kisheria kumzuia mtu yoyote kuingia katika uchaguzi.

Hata hivyo mwanasheria wa Makamu huyo wa Rais , Niyi Akintola amesema kuwa watakata rufaa haraka

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com