LAGOS:Atiku Abubakar kupepea bendera ya chama cha upinzani katika uchaguzi ujao Nigeria | Habari za Ulimwengu | DW | 21.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LAGOS:Atiku Abubakar kupepea bendera ya chama cha upinzani katika uchaguzi ujao Nigeria

Chama cha upinzani nchini Nigeria Action for Congress kimemchagua makamu wa rais Atiku Abukar kuwa mgombea wake katika uchaguzi wa mwakani.

Hatua hii imekuja baada ya rais Oleseguna Obasanjo kumzuia bwana Atiku kugombea uchaguzi huo kwa tiketi ya chama tawala.

Wachambuzi wa masuala yakisiasa nchini Nigeria wanasema kwamba hatua hiyo inaweza kutumiwa na rais Obasanjo kukitangaza kuwa wazi kiti cha makamu wa rais na huenda ikazusha mzozo wa kikatiba kuelekea uchaguzi mkuu kwenye taifa hilo la Afrika lenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com