LAGOS : Mtoto wa miaka 3 aendelea kushikiliwa mateka | Habari za Ulimwengu | DW | 08.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LAGOS : Mtoto wa miaka 3 aendelea kushikiliwa mateka

Wateka nyara wa Nigeria bado wanaendelea kumshikilia msichana wa Uingereza mwenye umri wa miaka mitatu Margaret Hill ambaye alibwakuliwa kutoka mji wenye kuzalisha mafuta wa Port Harcourt siku tatu zilizopita.

Mama wa mtoto huyo ambaye ni mwanamke wa Nigeria Oluchi Hill ameliambia shirika la habari la AFP huku akilia kwamba mtoto wake huyo bado yuko na wateka nyara hao ambao walikuwa wamempigia simu na kuweza kusikia kwa mbali sauti ya kulia ya mtoto wake huyo akiwasihi wamruhusu mama yake akamchukuwe.

Oluchi alisema hapo jana watekaji wake walidai kulipwa fedha za kumgombolea mtoto huyo ikiwa ni siku moja baada ya kutishia kumuuwa iwapo baba yake hatojitokeza kwenda kuchukuwa nafasi ya mtoto huyo jambo ambalo polisi imelipinga.

Polisi ya Nigeria imesema kwamba mtoto huyo Margaret yumkini akaachiliwa katika kipindi kisichozidi masaa 24.

Rais wa Nigeria Umaru Yar’adua pia ameiingilia kati kushinikiza kuachiliwa kwa mtoto huyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com