1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Labour yashinda viti vya ubunge ngome ya Conservative

21 Oktoba 2023

Chama tawala cha Uingereza cha Conservative, kimepoteza viti viwili vya ubunge dhidi ya chama cha upinzani cha Labour katika uchaguzi uliofanyika katikati mwa Juma hili.

https://p.dw.com/p/4Xq7V
UK Treffen der Konversativen Partei in Manchester | Premierminister Rishi Sunak
Picha: Hannah McKay/REUTERS

Chama tawala cha Uingereza cha Conservative, kimepoteza viti viwili vya ubunge dhidi ya chama cha upinzani cha Labour katika uchaguzi uliofanyika katikati mwa Juma hili. Matokeo hayo yanatizamwa kama mtihani mwingine kwa waziri Mkuu Rishi Sunak na chama chake tawala kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.

Labour ilipata ushindi katika uchaguzi mdogo kwenye maeneo mawili ambayo kijadi yamekuwa ngome ya Conservative ya Tamworth na Mid Bedfordshire. Matokeo hayo yameongeza matumaini ya chama cha Labour ya kurejea mamlakani baada ya kuwa upinzani kwa takriban miaka 14. Majimbo hayo yalikuwa wazi baada ya wabunge wake kujiondoa, ikiwemo mmoja aliyekumbwa na kashfa ya ngono.

Uchumi mbaya wa Uingereza, mgogoro mbaya zaidi wa kupanda gharama za maisha, pamoja na migogoro iliyokiandama chama cha Conservative kwa miaka kadhaa imechangia matokeo hayo.