1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yaifyatulia Ukraine makombora 57 pamoja na droni

Lilian Mtono
24 Machi 2024

Urusi imeifyatulia Ukraine makombora 57 pamoja na droni mapema hii leo, huku ikiushambulia mji mkuu Kyiv na mkoa wa Lviv ulioko magharibi mwa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4e4Mo
Mji wa Kyiv washambuliwa na Urusi
Milipuko ikwa inaonekana kwenye mji mkuu Kyiv nchini Ukraine wakati Urusi ilipokuwa ikiishambulia Machi 24, 2024. Picha: Gleb Garanich/REUTERS

Poland imearifu kuwa moja ya makombora hayo yaliyofyatuliwa na Urusi kuelekea Ukraine kwa kiasi fulani lilivunja kanuni zake za usalama wa anga.

Jeshi la Ukraine hata hivyo liliharibu makombora 18 kati ya 29 na droni 25 kati ya 28, hii ikiwa ni kulingana na jeshi hilo kwenye taarifa yake kupitia mtandao wa Telegram.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkuu wa utawala wa kijeshi mjini Kyiv Serhiy Popko, imesema milipuko kadhaa iliitikisa Kyiv mapema leo na Vikosi vya ulinzi wa anga vya Ukraine vimeharibu makombora kadhaa.

Urusi imekuwa ikiishambulia vikali Ukraine kwa siku kadhaa sasa, katika mashambulizi yanayotajwa na Moscow kama ya kisasi dhidi ya mashambulizi yaliyofanywa na Ukraine ilipokuwa ikifanya uchaguzi.