Kuvamiwa msikiti Islamabad | Magazetini | DW | 11.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Kuvamiwa msikiti Islamabad

Msikiti mwekundu huko Islamabad,Pakistan mwishoe umevamiwa na idadi kadhaa ya watu wameuwawa.

Uchambuzi wa wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo umetuwama zaidi juu ya mada mbili:

Kuvamiwa kwa msikiti mwekundu mjini Islambad,Pakistan na mabishano yaliozuka nchini Ujerumani kabla mkutano wa kilele juu ya jinsi ya kuwajumuisha wageni waisho humu nchini katika jamii ya wajerumani.

Gazeti la FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND ammbalo linazungumzia kinyan’ganyiro cha madaraka baina ya rais Musharrf na vyama vya upinzani nchini.Laandika:

“Katika kinyan’ganyiro hiki cha madaraka paned zote mbili tena na tena zikiegemea waumini wenye itikadi kali za kiislamu.Kwamba rais Musharaff akisitasita muda mrefu sasa kulin’goa shina la waislamu wenye itikadi kali ,ikielezwa mara kwa mara kuwa idara za usalama zikiungamkono msikiti huo mwekundi ingawa kisirisiri.Jinsi ilivyo hatari kufanya hivyo,kumedhihirika hivi sasa katika bahari ya damu iliozuka mjini Islamabad.Itikadi kali inaichimbia kaburi Pakistan kuizika kutoka ndani.”

Laandika Financial Times.Nalo Frankfurter Allgemeine Zeitung linaongeza:

” Serikali ya Musharraf kwa njia ya kutisha sana itagawa vidonge vya sumu ambavyo ilikuwa vigawiwe watu wengine kumeza.

Watalibani wa nchini Afghanistan na wa sehemu ya Pakistan kwa miaka mingi sasa tena kwa msaada wa idara za serikali za Pakistan wamegeuka kuwa turufu za kisiasa katika eneo hilo.Hata katika vita dhidi ya hasimu mkubwa India ,Pakistan haikujali kufumbia macho pale wapiganaji wa kiislamu wakivuka mpaka na kushambulia sehemu ya India ya Kashmir.”

Mod. Katika gazeti la NEUEN DEUTSCHLAND linalochapishwa Berlin tunasoma:

” Rais wa Pakistan ameanzisha mchezo wa kumwaya damu mjini Islamabad ili kuiyakinisha Marekani jinsi alivyovinjaribarabara kupambana na wenye itikadi kali .Kwani, ni marekani inayompa mabilioni ya dala na inataka kuona mafanikio katika vita dhidi ya wataliban .

Pia anataka Musharraf kuonesha mafanikio kwa umma wake kabla ya uchaguzi ujao mwishoni mwa mwaka huu.Unaweza kusema aliewasha moto ndio anaezima moto.Kwani kwa miezi kadhaa Musharaff akitumbua macho tu kuangalia yanayopita katika msikiti mwekundu.”

Mod.Ni maoni ya NEUEN DEUTSCHLAND:

Gazeti la STUTTGARTER ZEITUNG linatoa kitisho na kuingiwa na wasi wasi kwamba:

” endapo Pakistan ikiangukia mikononi mwa waislamu wenye itikadi kali,basi bomu la atomiki la Pakistan litaangukia pia mikononi mwao.Hapo kiyama kitadhihirika.Hata vita nchini Irak havikufaulu.Na wamarekani wakiaanza kweli kufunga virago kuihama Irak,hapo tena wapiganaji jihadi katika ulimwengu mzima wa kiislamu watashajiishwa kuimarisha vita dhidi ya kambi ya magharibi…”

Juhudi za serikali ya Ujerumani kuwaleta pamoja wakaazi wake wa kigeni karibu na jamii ya wajerumani zimepata pigo.Jumuiya nyingi za wakaazi wa kituruki humu nchini, zimeahidi kuhudhuria tu mkutano wa kilele alioitisha kanzela Angela Merkel hapo kesho ikiwa tu Kanzela ataridhia kufanya mageuzi katika sheria ya uhamiaji nchini.Msemaji wa serikali, lakini amelipinga pendekezo hilo.Gazeti la WESTDEUTSCHE ZEITUNG kutoka Düsseldorf laandika:

” Mwaka mmoja uliopita ilikua furaha ilioje juu ya mpango huu.Kanzela Merkel aliueleza mkutano uliopita wa kilele ni “tukeo la kihistoria.”Miezi 12 baadae,matokeo yake hayatii moyo.Kwani, jumuiya nyingi za kituruki zinakutumia kubana zaidi sheria za uhamiaji humu nchini kwa jamaa zao sababu ya kueneza sumu juu ya mkutano huo. “