1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya maoni kuhusu katiba Kenya kufanyika kesho

Josephat Nyiro Charo3 Agosti 2010

Usalama umeimarishwa kote nchini Kenya hasa katika maeneo yaliyo ngome ya wafuasi wanaoipinga katiba mpya

https://p.dw.com/p/Oani
Usalama umeimarishwa kuzuia kutokea machafuko kama haya ya baada ya uchaguzi wa 2007Picha: AP

Kenya inajiandaa kuipigia kura ya maoni rasimu ya katiba mpya hapo kesho Jumatano.Usalama umeimarishwa kote nchini humo hasa katika maeneo ya Mkoa wa Bonde la Ufa ambako kulizuka ghasia baada ya uchaguzi mkuu wa Disemba mwaka 2007.Katiba hiyo mpya ni sehemu ya mageuzi ya kisiasa yaliyo na azma ya kuzuwia ghasia kutokea wakati wa uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika mwaka 2012.

Shughuli nzima itasimamiwa na kiasi ya waangalizi zaidi ya alfu moja wa Jumuiya ya Madola,Commonwealth na Shirika la maendeleo ya Kikanda,IGAD.Kwa mara ya kwanza, matokeo ya kura hiyo yatatangazwa kutumia huduma za mtandao na simu za mkononi.

Ili kupata sura kamili ya maandalizi hayo mwandishi wetu wa Nairobi Alfred Kiti ametuandalia ripoti ifuatayo.

Mtayarishaji:Alfred Kiti

Mpitiaji:Thelma Mwadzaya