1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kumbukumbu ya mashumbilizi ya Mumbai

26 Novemba 2009

<p>Nchini India leo ni kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu yale mashambulizi ya kigaidi katika mji wa Mumbai, wenye shughuli ya kifedha, yaliyosababisha umwagikaji mkubwa wa damu.

https://p.dw.com/p/KgkP
People stand around a damaged vehicle at the site of an explosion in Mumbai, India, Wednesday, Nov. 26, 2008. unmen targeted luxury hotels, a popular tourist attraction and a crowded train station in at least seven attacks in India's financial capital Wednesday, wounding 25 people, police and witnesses said. A.N Roy police commissioner of Maharashtra state, of which Mumbai is the capital, said several people had been wounded in the attacks and police were battling the gunmen. "The terrorists have used automatic weapons and in some places grenades have been lobbed," said Roy. Gunmen opened fire on two of the city's best known Luxury hotels, the Taj Mahal and the Oberoi. They also attacked the crowded Chhatrapati Shivaji Terminus station in southern Mumbai and Leopold's restaurant, a Mumbai landmark. It was not immediately clear what the motive was for the attacks. (AP Photo)
Watu wakishuhudia kitendo cha kigaidi hapo Mumbai, tarehe 28 Novemba 2008Picha: AP
  Kundi la watu kumi waliokuwa na bunduki, walifanya mashambulizi ambayo ndiyo mabaya kabisa katika historia ya nchi hiyo. Sherehe mbali mbali zimepangwa ikiwemo, gwaride la polisi kuonyesha ishara ya nguvu za vikosi vya usalama, huku India ikiwakumbuka watu 166 waliouawa katika shambulizi hilo.

Ni shambulizi lililozidisha zaidi mgogoro kati ya majirani wawili Pakistan na India- hasa ilipobainika kundi linaloitwa Lashkar e Taiba lenye makao yake Pakistan ndilo lililopanga uvamizi mjini Mumbai.

Na huku India leo, ikikumbuka- wanaendelea kuiwekea mbinyo serikali ya Pakistan kukabiliana na makundi yenye siasa kali humo, kwa kile wengi wanasema Pakistan imeregea katika kuangamiza vitisho vya makundi hayo.

Mtaalamu wa maswala ya usalama kutoka India, Waslekar Sundeep anasema

'' Utawala wa Pakistan kwa muda mrefu umekuwa ukiuunga mkono kwa siri ukishirikiana makundi ya kigaidi nchini humo. Na pia wana maslahi yao- na maslahi yao ni kujenga sura ya wasiwasi. Kwa sababu ugaidi kwa ujumla huwa ni kuzusha machafuko.''

Polisi nchini India wanashika doria katika mji wote wa Mumbai, huku wakionyesha zana zao za kisasa- ishara kwamba wako imara kwa lolote. Wabunge, na wachezaji cricket pia walijumuika na raia wengine nchini India kuweka mashada ya maua na kujumuika katika maombi kuwakumbuka watu 166 waliouawa katika shambulizi hilo.

Mishumaa iliwashwa katika Sinagogi moja ya  Mumbai. Viongozi wa kidini, wanadiplomasia wa kimataifa waliungana na raia wa India, katika makumbusho hayo, wakitoa mwito wao amani na umoja katika kupigana na kuangamiza makundi ya kigaidi kote duniani.

Akiwa ziarani nchini Marekani, Waziri mkuu wa India Manmohan Singh aliitolea changamoto serikali ya Pakistan kufanya kila juhudi kuonyesha mkono wake wa sheria una nguvu, dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya kigaidi nchini humo, ambao bado huru kutekeleza mashambulizi katika eneo hilo.

Premierminister Manmohan Singh
Waziri Mkuu wa India Manmohan SinghPicha: Fotoagentur UNI

Mwaka mmoja uliopita magaidi kumi waliuvamia mji wa Mumbai, katika shambulizi lililoitikisa nchi hiyo na kuushtua ulimwengu mzima. Ulimwengu mzima ulibakia mdomo wazi, pale picha za shambulizi hilo lililodumu kwa siku tatu, zilipeperushwa moja kwa moja katika televisheni kote duniani.

Kati ya washambulizi wote kumi ni mmoja tu ndiye aliyebaki hai, raia wa Pakistan ambaye tayari ameshtakiwa kwa mauaji. Jana mahakama ya kupambana na ugaidi nchini Pakistan iliwafungulia mashtaka watu sita kwa kuhusika na mashambulizi ya Mumbai. Wote lakini walikanusha mashtaka hayo.

Mwandishi: Munira Muhammad/ AFPE:

Mhariri: Abdul-Rahman