Kuhamishiwa kwa mtuhumiwa wa ugaidi wa Kenya huko Guantanamo
28 Machi 2007Matangazo
Abdul Malik anatajwa kuhusika na shambulio la hoteli ya Mombasa lililouwa zaidi ya watu 12 hapo mwaka 2002 na jaribio la kudungua ndege ya Israel iliokuwa na abiria 271 karibu na Mombasa.
Mohamed Dahman alipata nafasi ya kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji ya tume hiyo Mwambi Mwaru ambaye anaielezea hatua hiyo ya serikali kuwa tata sio halali, inavunja haki za binaadmau, sheria za Kenya na za kimataifa.