1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kosovo yakaribia kutangaza uhuru.

8 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CmRX

Pristina.

Vyama hasimu katika jimbo linalotaka kujitenga la Kosovo wamefikia makubaliano ya kugawana madaraka ili kuunda serikali. Ushirika baina ya chama cha kiongozi wa zamani wa waasi Hashim Thaci na mpinzani wake mkubwa , chama cha Democratic League of Kosovo, wanatarajiwa kupigiwa kura kesho Jumatano. Kosovo inaonekana kutangaza uhuru baada ya uchaguzi wa rais nchini Serbia mwezi February katika hatua ambayo inapingwa vikali na Serbia na Urusi. Wakati huo huo , umoja wa Ulaya unatarajiwa kufanya uamuzi juu ya kutuma ujumbe ili kuchukua nafasi ya ujumbe wa umoja wa mataifa ambao ulikuwa unaendesha utawala wa jimbo hilo la Kosovo tangu mwaka 1999.