1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kusini yapata rais mpya

20 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdwC

SEOUL

Mkuu wa zamani wa kampuni Lee Myung-bak atakuwa rais mpya wa Korea Kusini baada ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi uliofanyika hapo jana.

Lee ambaye kampeni yake ya uchaguzi ilikumbwa na madai ya kashfa za hujuma ameahidi kusaidia biashara na kuwa na msimamo mkali dhidi ya Korea Kaskazini.

Marekani imempongeza Lee kwa ushindi huo na kusema kwamba inasubiri kwa hamu kushirikiana na serikali yake mpya baada ya kuzinduliwa mapema mwakani.