Kombe la shirikisho; Leverkusen chali
13 Februari 2014Matangazo
Jana timu ya daraja la pili ya Kaiserslautern iliiondoa Bayer Leverkusen katika kinyang'anyiro cha kombe la shirikisho la Ujerumani DFB Pokal katika mchezo wa robo fainali, baada ya kushinda kwa bao 1-0 katika mchezo ambao ulichezwa kwa muda wa dakika 120 baada ya timu hizo kutoka sare bila kufungana katika muda wa kawaida.
Wolfsburg iliishinda nguvu Hoffenheim kwa mabao 3-2 na Bayern Munich ilidhihirisha ubabe wake kwa kuishinda Hamburg kwa mabao 5-0.
Timu nne Wolfsburg, Kaiserslautern, na Bayern Munich zimeingia nusu fainali ambapo Borussia Dortmund ilikuwa timu ya kwanza kukata tikiti yake kwa kuishinda Eintracht Frankfurt kwa bao 1-0 siku ya Jumanne.