Kombe la klabu bingwa Afrika | Michezo | DW | 23.04.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kombe la klabu bingwa Afrika

Timu 7 za Afrika kaskazini zimetamba katika dutu ijayo na kuiachia ASEC Abidjan pekee nafasi moja katka zahama za kombe la klabu bingwa. Martin Lel wa Kenya awika tena katika London marathon na schalke yaparamia tena kileleni mwa Bundesliga:

Cacau azika Bayern Munich kwa mabao yake 2

Cacau azika Bayern Munich kwa mabao yake 2

Natuanze na Ligi mashuhuri barani Ulaya:

Inetr Milan ya Itali imetawazwa tayari mabingwa wa Itali baada ya kuikomea jana Siena mabao 2:1-huku mabao yote yakitiwa na jogoo wa Itali katika kombe la dunia Marco Materazzi.Kwa kuwa AS Roma, iliopo nafasi ya pili ya ngazi ya Ligi ilikomewa mabao 2:1 na Atlanta,Inter Milan ilitawazwa na mapema mabingwa wa Itali wakiongoza mwanya wa pointi 16 kileleni ingawa kuna mechi 5 zaidi kuchezwa.Kwa Inter zimegeuka ada.

Katika Bundesliga-Ligi ya Ujerumani,Schalke 04 imeunyakua tena usukani wa Ligi hapo jumamosi baada ya ushindi wa mabao 2:0 dhidi ya Energie Cottbus.Mabingwa Bayern Munich lakini waliteleza tena katika changamoto yao ya kufa-kupona kati yao na Stuttgart.

Stuttgart imein’gan’gania nafasi ya tatu ya ngazi ya Ligi nyuma ya Schalke na Werder Bremen ilipoizaba Munich mabao 2:0.

Akielezea pigo hilo walilopata stadi wa kiungo wa Bayern Munich kutoka Holland,Van Buemel alisema:

“Tulivinjari kweli kutamba leo ,lakini ghafula tulitiwa bao la kipumbavu kabisa na yasikitisha kutiwa bao kama lile na mara ikawa mabao 2:0.Hapo tena mambo yakawa magumu kurejea tena katika m chezo.Tulijaribu,lakini haikutosha.”

Stadi wa mpambano huo alikua mbrazil aitwae Cacau

Ambae alilifumania lango la Bayern munich mara 2 tena katika muda mfupi.Alisema,

“Tumetamba barabara tukicheza ari moja timu moja.Huo ukawa ushindi mkuu kabisa na timu yetu ilistahiki ushindi huo”

alidai Cacu baada ya mabao yake 2 ambayo pengine, yamepiga msumari wa mwisho katika jeneza la Bayern Munich baada ya kutolewa katika kombe la Taifa,kombe la klabu bingwa barani ulaya na sasa yavuliwa taji katika Bundesliga.Kocha wa Munich, Ottmar Hitzfeld amewaonya sasa wachezaji wake katika kiako cha saa 1.5 kuwa kwa wengi wao siku zao katika Bayern munich zimemalizika ikiwa wataendelea kucheza kama jumamosi walipozabwa 2:0 na stuttgart.

Katika PREMIER LEAGUE-Ligi ya Uingereza hakujazuka badiliko lolote kileleni katika mbio za farasi 2 Manchester united na Chelsea.Manchester iliilaza ngoma uporo ilipozimwa sare bao 1:1 na Middlesbrough wakati Chelse walitoka pia sare 0:0 na New Castle jana.

Huko Ufaransa Olympique nayo ilitoroka na taji lake la 6 hata kubidi kuingia uwanjani,kwani timu iliopo nafasi ya pili ya ngazi ya Ligi Toulouse kulazwa kwa mabao 3-2.

Ama katola La Liga-ligi ya Spian ,FC Barcelona walikiona jana kile kilichomtoa kanga manyoya:

Villarreal iliizaba Barcelona na Ronaldinho wao mabao 2:0.Hata hivyo, Barcalona yaongoza bado Ligi ya Spain ingawa kwa pointi 1.

Katika kinyan’ganyiro cha kombe la klabu bingwa barani Afrika,ASEC Abidjan ya Ivory Coast ilizima mkumbo wa timu za Afrika ya kaskazini kumiliki pekee yao nafasi 8 za mwisho za kinyan’ganyiro hicho kwa kufaulu kutoka suluhu 0:0 jana na Wydad casablanca na hivyo kuondoka na ushindi wa mabao 2:0 kufuatia duru zote mbili.

Mikwaju 2 ya penalty katika kipindi cha pili yaliotiwa na Salem Rewani yalitosha kuipeperusha timu nyengine ya kaskazini Al Ittihad ya Libya n kuipiga kumbo Etoile du Congo.Tayari jumamosi Esperence na etoile Sahel zilijiunga na duru hiyo ya robo-finali na kufuatwa na Etoile du sahel.Pia Royal Armed Forces ya morocco imeingia duru hiyo.Hapo ijumaa timu 3 za Afrika ya kaskazini mabingwa Al Ahly,JS Kabylie ya Algeria na Al hilal ya Sudan zilitamba na kuondoka na tiketi zao .

Huko Mwanza Tanzania-Esperence ya Tunisia iliwasilina mabao 3 kikapuni kama zawadi iliopewa na young Africana walipowatembelea nyumba.katika ziara yao ya jumamosi huko Mwanza,Young Africans hawakuwa na zawadi mara hii kwani majogoo wote wawili wa shamba na mjini, walipomudu suluhu 0:0.

Katika mbio za London marathon jana alikua mkenya Martin Lel alietamba na sio binbwa wa rekodi ya dunia mkenya mwenzake Paul Tergat wala bingwa wa zamani wa masafa marefu Haile Gebreselassie wa Ethiopia.

Martin Lel alizima vishindo vya mmorocco Abderrahim Goumri na kama mwaka 2005 alitorika na taji la London marathon kwa muda wake wa masa 2:07.41.

Katika upande wa wanawake, mkenya Lornah Kiplagat anaekimbia chini ya bendera ya Holland,aliongoza kitambo kirefu lakini bingwa wa Asia kutoka China, Zhou Chunxiu alimwambia kutangulia si kufika.Muethiopia Wami alimfuata nafasi ya pili.

 • Tarehe 23.04.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcI
 • Tarehe 23.04.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcI