kombe la afrika la mataifa | Michezo | DW | 26.03.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

kombe la afrika la mataifa

Tanzania yazabwa mabao 4:0 na Senegal wakati Nigeria yaondoka na ushindi wa bao 1:0 dhidi ya Uganda.Angola,Ivory Coast na mabingwa Misri zote zaondoka na ushindi.

Kuranyi afumania lango la Czch mara 2.

Kuranyi afumania lango la Czch mara 2.

Baada ya Ujerumani kuizaba Jamhuri ya czech mabao 2-1 jumamosi katika kinyan’ganyiro cha kombe la ulaya la Mataifa,kocha Joachim Loew, ameamua kutowachezesha nahodha Michael Ballack na wachezaji wengine 8 maarufu katika dimba la kirafiki jumatano ijayo Ujerumani ikipambana na Denmark.

Kocha Loew amewaita wachezaji 2 wapya kwa timu ya taifa hapo jana –mshambulizi chipukizi wa FC Cologne inayocheza daraja ya pili ya Bundesliga-Patrick Holmes na mchezaji wa kiungo Simon Rolfes wa Bayer Leverkusen.

Ujerumani sasa takriban imeshatia mfukoni tiketi yake ya kwenda mwakani Uswisi au asustria kwa Kombe la Ulaya baada ya ushindi wa mabao 2:1 dhidi ya Czech mjini Prague.Alikuwa Kevin Kuranyi alieachwa nje ya Kombe la dunia mwaka jana, alieufumania mara 2 mlango wa Jamhuri ya Czeck.Kwa mabao hayo 2 Kevin Kuranyi,mjerumani wa asili ya Brazil amethibitisha kwamba amestahiki sasa kurejea katika timu ya Taifa.Binafsi alisema:

“Bila shaka , ilikua kupiga hatua mbele kwangu .Nafurahi kuweza kuisaidia timu ya Taifa na nitajaribu kuendelea kufuata mkondo huo.”

Mwishoni mwa wiki ilikua duru nyengine ya kinyan’ganyiro cha kuania tiketi za finali ya mwakani ya Kombe la Afrika la mataifa nchini Ghana.Angola na Ivory Coast zilipiga hatua karibu sana kutia mfukoni tiketi zao za Accra.Angola ilishinda mpambano wake 3 mfululizo kwa kuizaba Eritrea mabao 6:1.Flavio aliipatia Angola pekee mabao 2.Sasa Angola inahitaji pointi 4 tu katika mapambano 3 yajayo kwenda Accra.

Ivory Coast iliocheza finali ya kombe lililopita na Misri ,inahitaji ushindi katika mechi ijayo kunyakua nayo tiketi yake ya Ghana.Kwani, Ivory Coast ilitandika Madagascar mabao 3:0 tena mjini Antananarivo hapo jana.Hata Nigeria ilitamba kama ilivyofanya Senegal na mabingwa Misri.

Tanzania ilikomewa mabao 4:0 na Senegal.

Changamoto kati ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Ethiopia mjini Kinshasa,ilibidi kuahirishwa kufuatia machafuko mjini Kinshasa yaliosababisha vifo vya watu kadhaa.Wakuu wa hospitali wamearifu zaidi ya watu 100 waliuwawa.Mabingwa Misri walikumta Mauritania mabao 3-0 mjini Cairo jana na wanaongoza kundi lao la pili wakijiwinda kutetea mwakani ubingwa wao.Morocco ilibidi kuridhika na sare tu ya bao1:1 na Zimbabwe .

RIADHA:

Mbio za ubingwa wa nyika ulimwenguni zilimalizika jumamosi mjini Mombasa kwa pigo kubwa kwa Ethiopia.Bingwa wao wa mbio hizi Kenenisa Bekele alisema alijitoa mashindanoni kutokana na maumivu ya mwili na kupoteza akili.Ushindi ulienda kwa Eritrea,Holland na Kenya .Lornah Kiplagat,mkenya mzaliwa wa Holland alinyakua ushindi upande wa wasichana.Hivyo amekuwa mzungu wa kwanza kushinda mbio hizo.Eritrea ilinyakua ushindi upande wa wanaume.Tadesse, alizima vishindo vya wakenya.

Na katika mbio za marathon za Taepei,China ya kizalendo,mkenya Irene Mogata alinyakua ushindi upande wa wasichana wakati mzimbabwe Abel Chimukoko alitamba upande wa wanaume.

 • Tarehe 26.03.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcT
 • Tarehe 26.03.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcT