1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Klopp azima rekodi ya Man City kutofungwa

Sekione Kitojo
15 Januari 2018

Pep Guardiola  awataka  wachezaji  wake  kujifunza  kutokana  na machungu  ya  mchezo dhidi  ya  Liverpool  jana  Jumapili.

https://p.dw.com/p/2qsYY
Fußball Premier League Liverpool - Manchester City
Sadio Mane (kulia) akikwamisha mpira wavuni dhidi ya Man CityPicha: picture-alliance/empics/P. Byrne

 

Manchester  City  katika  Premier League  nchini  England imeshuhudia  rekodi  yake  ya  kutofungwa  ikisitishwa  jana  Jumapili wakati  FC Liverpool  iliweka  kando  kuondoka  kwa  mchezaji  wake nyota  wa  kati  Philippe  Coutinho  na  kupata  ushindi  mtamu  wa mabao 4-3.

Premier League FC Liverpool Jürgen Klopp & Philippe Coutinho
Jurgen Klopp akimuelekeza mchezaji wake wa zamani Philippe Coutinho aliyehamia BarcelonaPicha: Getty Images/M. Regan

Arsenal  ambayo  inasua sua  msimu  huu  ilikubali  kipigo  cha mabao 2-1 dhidi  ya  Bournemouth , wakati  matatizo  ya  kocha Arsene  Wenger  yakizidi  kutokana  na  kukaribia  kuondoka  katika kikosi  hicho  mshambuliaji  nyota  Alexis Sanchez. Kwingineko Chelsea  ilishikwa  shati  na  kutoka  sare  ya  bila  kufungana  na Leicester City  wakati  Harry Kane   wa  Tottenham  amevumisha kimbunga  na  kufunga  mabao  mawili  katika  ushindi  wa  mabao 4-0  dhidi  ya  Everton  na  West Bromwich Albion  ilipata  ushindi wake  wa  kwanza  katika  Premier League  kwa  kuishinda  Brighton kwa  mabo 2-0.

Kocha  mkuu  wa  Machester  City Pep Guardiola  amewapa changamoto  wachezaji  wake  kutumia  kipingo  walichopokea kutoka  kwa  Liverpool  cha  mabao 4-3  kuwa  ni  tahadhari  ya kujilinda  dhidi  ya  kubweteka. Kikosi  cha  Guardiola  kilipokea kipigo  dhidi  ya  Liverpool  na  kusitisha  rekodi  yao ya  kutofungwa  katika  Premier League  iliyfikia  mwisho  katika  uwanja  wa  Anfield.

Fußball Gestik Trainer Pep Guardiola
Pep Guardiola kocha wa Manchester CityPicha: picture-alliance/empics/A. Devlin

Licha  ya  mabao  ya  dakika  za  mwisho  ya  Bernardo Silva  na Ilkay  Gundogan  yaliyoweka  heshima  kidogo  katika  muonekano  wa matokeo  hayo, lakini  kocha  huyo  wa  Man City  Guardiola  hakuwa na  malalamiko  juu  ya  kikosi  chake  kupata  kipigo  cha  kwanza tangu  Aprili  5  dhidi  ya  Chelsea.

Kocha wa Liverpool  Jurgen Klopp  anaamini  kwamba  mchezo  huo  ulikuwa  bora  kabisa  msimu  huu , umeonesha  haja  ya kutohofia wakati  timu inapokumbana  na  timu  yenye uwezo  mkubwa  kama  City.

Mwandishi: Sekione  Kitojo  / afpe / rtre / ape /

Mhariri: Yusuf , Saumu