1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kivumbi cha kombe la mataifa ya bara Afrika kung'oa nanga wikendi hii

Nchi za Guinea ya Ikweta na Gabon yatawakaribisha wageni wengi kuanzia wiki ijayo huku kivumbi cha fainali za kombe la mataifa ya bara Africa maarufu kaam Orange Africa Cup of Nations kiking'oa nanga jumamosi.

Mchezaji wa Ghana John Mensah

Mchezaji wa Ghana John Mensah

Timu zitakazo shiriki tayari zinaendelea na kujinoa makali na kupata maarifa ya mwisho mwisho kwa kucheza michuano ya kirafiki katika sehemu mbalimbali kabla ya kusafiri hadi kwa nyumbani kwa wenyeji wao. Wakufunzi wa timu mbalimbali wameonyesha matumaini yao ya kudhihirisha usogora wao katika dimba hilo kubwa barani Afrika. Kocha wa Moroco Eric Gerets ameelezea matumaini ya kutwaa kombe hilo mwaka huu baada ya matayarisho yake kwenda vyema nchini Uhispania. Naye mwenzake wa Tunisia Sami Trabelsi amesema anataraji kuwa vijana wake wa Carthage Eagles wataonyesha mchezo mwema baada ya vijana hao kuzamishwa na Cote dIvoire mbili bila katika mchuano wa kujipima nguvu kule Abu Dhabi.

Matokeo ya mechi za ligi ya Primia nchini Uingereza

Katika mkusanyiko wa matokeo ya mechi zilizosakatwa mwishoni mwa wiki barani Ulaya, nchini Uingereza katika Primia League mabingwa Manchester United waliwaduwaza Bolton kwa kuwafunga tatu bila na hivyo kutoshana kwa alama na viongozi Manchester city ambao wanakutana na Wigan hii leo. Nambari tatu Tottenham Hotspurs walikosa nafasi ya kufukuzana na vilabu hivyo viwili vya Manchester wakati walipotekwa sare ya kufungana bao moja nyumbani na Wolverhampton Wanderers. Chelsea waliwapiku Sunderland ili kusalia katika nafasi ya nne nayo matumaini ya Arsenal kufuzu kwa ligi ya mabingwa yakapata pigo wakati waliponyamazishwa mabao matatu kwa mawili na Swansea.

Wachezaji wa Barcelona wakisherekea bao

Wachezaji wa Barcelona wakisherekea bao

Katika La Liga viongozi Real Madrid na nambari Mbili Barcelona walipata ushindi mgumu dhidi ya Real Mallorca na Real Betis mtawalia na walionekana kutoridhisha kabla ya mchuano wao wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya wa kombe la Mfalme utakaosakatwa jumatano hii. Vijana wa Jose Mourinho walitoka nyuma na kuwashinda Mallorca mbili moja huku nao BARCELONA wakikubali kufungwa mabao kwa mara ya kwanza nyumbani katika ligi msimu huu wakati walipoishinda Betis magoli nne kwa mawili.

Inter Milan imeweka mezani toleo la pauni milioni 20.7 ili kupata huduma za mchezaji Carlos Tevez, lakini huenda isifikie kiwango cha tathmini ya klabu ya Manchester City kwa mchezaji huyo. Rais wa Inter Massimo Moratti amesema toleo lao ni euro milioni 25 na sasa itawahusu Man City ikiwa watakubali au la. AC Milan walijiondoa katika mazungumzo ya kumsajili Tevez mwenye umri wa miaka 27 alhasimi iliyopita, baada ya mchezaji Alexander Pato kudinda kujiunga na Paris St Germain.

Bundesliga kurejea tena Ijumaa hii baada ya likizo ya mwezi mzima

Hapa nchini Ujerumani ligi ya taifa ya soka Bundesliga inarejea tena kwa kishindo ijumaa hii baada ya kipindi cha takriban mwezi mmoja wa mapumziko. Bayern ilimaliza nusu ya kwanza ya ligi ikiwa kileleni na imejiandaa kupata ushindani mkali kutoka kwa mahasimu wake Borussia Dortmund ambao kwa sasa wako katika nafasi ya pili na pia Schalke 04 wanaoshikilia nafasi ya tatu. Timu zote za ligi zinarejea kutoka likizoni ambako walisafiri katika sehemu nyingi ili kufanya mazoezi na kijinoa kabla ya kuendelea na nusu ya pili ya ligi.

Na Diego Maradona amefanyiwa upasuaji wa figo katika hopsitali moja kule Dubai ambako amekuwa akitibiwa. Msemaji wa Hospitali hiyo amesme akupitia taarifa kuwa nahodha huyo wa zamani wa timu ya Argentina iliyoshinda kombe la dunia mwaka 1986 ambaye sasa ni kocha wa timu ya Al Wasl katika umoja wa Milki za kiarabu ataruhusiwa kuondoka hospitalini katika muda wa saa chache zijazo baada ya upasuaji wa kufana. Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 51 ambaye alioongoza timu ya taifa ya Ujerumani katika dimba la kombe la dunia mwaka 2010 amekuwa na matatizo kadhaa ya kiafya kwa miaka kadhaa ikiwa ni pamoja na wakati alipomaliza siku kumi hospitalini akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi akiwa na matatizo ya moyo na kupumua mnamo mwaka 2004.

Mwandishi: Bruce Amani

Mhariri: Yusuf Saumu

 • Tarehe 16.01.2012
 • Maneno muhimu Michezo
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13kZE
 • Tarehe 16.01.2012
 • Maneno muhimu Michezo
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13kZE