Utalii wa kimazingira Kaskazini mwa Ujerumani
17 Novemba 2015Matangazo
Kwa wajerumani, utalii katika miradi ya mazingira imekuwa kama tabia kwa wengi, na tabia hiyo husaidia kuweka uelewa na hamasa ya kila mmoja kuyalinda mazingira na viumbe asilia wanaoishi katika mazingira hayo.
Sehemu moja yenye vivutio vingi vya kimazingira ni mji wa Norddeich, ambao idhaa yako ya Kiswahili iliutembelea hivi karibuni. Tafadhali sikiliza makala hii ya Sura ya Ujerumani iliyoandaliwa kutokana na ziara hiyo.
Inahusu matunzo ya ufukwe wa tope katika Bahari ya Kaskazini, na Kituo cha kuwatunza mayatima wa wanyama wa majini waitwao sili, au seals kwa lugha ya kiingereza. Makala hiyo imeandaliwa nami Daniel Gakuba.