Kitisho cha mgomo wa reli | Magazetini | DW | 07.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Kitisho cha mgomo wa reli

Mtoto wa waziri mkuu wa zamani wa Bavaria Franz Josef-strauss-Max Strauss hajakutikana na hatia ya kukwepa kulipa kodi.Mgomo wa reli huenda ukafanyika au kuepushwa ?

Uchambuzi wa wahariri wa magazeti ya leo ya Ujerumani, umetuwama hasa juu ya mada 2: Kwanza hukumu ya kutokutikana na hatia motto wa waziri mkuu wa zamani wa Bavaria-Max Staruss kuwa alikwepa kulipa kodi za mapato.Mada ya pili, ni mvutano juu ya nyongeza za mishahara kati ya madereva wa reli na shirika la reli la Ujerumani-Deutschen Bahn.

” Muda mrefu wajerumani wakitikisa kichwa wanaposikia wafanyikazi wa mashirika ya reli nchini Uingereza,Itali na Ufaransa wanagoma.Dereva wa treni nchini Ujerumani mara nyingi huwa ni mtumishi wa serikali na hivyo kugoma ilikua mwiko.

Lakini nafasi yake ya kazi ilikua ya uhakika.Sasa haistaajabishi kuona hasa madereva wenye ujuzi maalumu au madaktari walioanguka mateka tangu wa malipo ya chini hata wa ukosefu wa uhakika wa nafasi zao za kazi,hawataki kuvumilia zaidi.”

Mod:Gazeti la Stuttgarter Nachrichten linadai pawepo mfumo mmoja wa mapatano kati ya waajiri na waajiriwa.Laandika:

“Shirika la madereva wa reli GDL linadai nyongeza ya kima cha hadi 31% na mabadiliko makubwa ya mfumo wa muda wa kufanya kazi.

Hii inaongoza wapi ? Je,kesho pia viongozi wa misafara ambao bila wao madereva wa treni hawawezi kuendesha treni zao,wakija mkudai mapatano yao pekee bila kuwahusu wengine itakuaje ?

Ama gazeti linalochapishwa mjini Bonn-General-Anzeiger linahisi laiti pangetumika busara na nia njema mzozo huu ungepatiwa zamani ufumbuzi na uongozi wa ICE.Gazeti laongeza:

Tena bila ya mgomo.Ilikua wazi kabisa kwamba madereva wa reli wanadai nyongeza ya mshahara.Ni wazi pia kuwa suluhisho la madai yao lazima lipatikane.Kwahivyo katika hali kama hiyo ni kutafuta muafaka na sio kila upande kudai makuu kupita kiasi.

Ni maoni ya busara ya General Anzeiger linalochapishwa mjini Bonn.

Liktugeuzia mada gazeti la DIE WELT linatukumbusha kuwa baada ya uchunguzi wa muda mrefu na duru nyingi mahkamani,motto wa mwanasiasa mashuhuri wa zamani Max Strauss amefutiwa mashtaka kuw alikwepa kulipa kodi za mapato.

Mahkama ya Augsburg haikuona ushahidi wowote kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 48 –mtototo wa waziri-mkuu wa zamani wa Bavaria-marehemu Franz Josef Strauss,malipo aliopokea kwa biashara yake hajayalipia kodi.

DIE WELT limegundua:

“Kinyume na Max Strauss, wengine walioshtakiwa pamoja nae wamepewa adhabu ya vifungo korokoroni.Kwa jicho la ukubwa wa mashtaka hayo,hukumu iliotolewa ni laini….”

Ama gazeti la Berliner-Zeitung linasisitiza kuwa hukumu iliotolewa ya kutomkuta na hatia mwana wa Strauss……

”ni pongezi zinazofaa kwenda kwa dola inayofuata sheria n a hii kabisan haiteremshi hadhi ya uchunguzi wa mawakili wa vyombo vya sheria na ya maafisa wanaowaandamama wakwepaji kodi.”