Kirusi kipya cha Ebola chauwa 16 nchini Uganda | Habari za Ulimwengu | DW | 30.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kirusi kipya cha Ebola chauwa 16 nchini Uganda

Kirusi kipya cha ugonjwa wa Ebola wenye kusababisha maafa kimewaambukiza watu 51 na kuuwa 16 katika eneo moja la Uganda karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo .

Dr.Sam Zaramba Mkurugenzi wa Huduma za Afya katika Wizara ya Afya nchini Uganda amesema kwenye taarifa kwamba mripuko wa ugonjwa huo huko Bundibugyo hivi sasa umethibitishwa kuwa ni Ebola.

Kirusi hicho kimeonekana kuwa sio kikali sana jambo ambalo sio la kawaida na waathirika wamekuwa hawavuji damu nyingi na wengi wao wamekufa kutokana na homa.

 • Tarehe 30.11.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CUwq
 • Tarehe 30.11.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CUwq

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com