1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kirkuk, Iraq.Polisi wafanyamsako wa nyumba kwa nyumba.

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD55

Maelfu ya polisi wa Iraq na wanajeshi wamefanya msako mkubwa wa nyumba kwa nyumba wakitafuta silaha na wapiganaji katika mji wa kaskazini wenye machimbo ya mafuta wa Kirkuk.

Kiasi cha watu 150 wamekamatwa na zaidi ya bunduki 220 zimekamatwa.

Wakaazi wote waliamriwa kutoonekana mitaani wakati marufuku ya kutotembea ikiendelea kuimarishwa.

Mjini Tal Afar , kaskazini magharibi ya mji wa Kirkuk, mtu mmoja aliyejitoa muhanga kwa kujilipua katika gari amewauwa watu 14 ikiwa ni pamoja na raia wanne katika shambulio dhidi ya kituo cha doria cha jeshi la Iraq.