1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kipruto avunja rekodi ya Kipchoge Tokyo

3 Machi 2024

Mwanariadha Benson Kipruto ashinda mbio za masafa marefu za Tokyo za wanaume kwa muda wa saa mbili, dakika mbili na sekunde 16, na kuvunja rekodi ya bingwa wa dunia Eliud Kipchoge katika mitaa ya mji mkuu wa Japan.

https://p.dw.com/p/4d73K
Eliud Kipchoge
Mwanariadha wa Kenya Eliud Kipchoge amaliza katika nafasi ya 10 katika mbio za masafa marefu Tokyo 2024.Picha: picture-alliance/augenklick/firo Sportphoto

Timothy Kiplagat alimaliza katika nafasi ya pili kwa kutimka kwa saa 2:02:55 na Vincent Ngetich akimaliza katika nafasi ya tatu kwa saa 2:04:18 wote wakiiwakilisha Kenya.

Kipchoge alikuwa akipambana kufikia rekodi ya muda ya 2:02:40 aliyoweka mwaka wa 2022, na bingwa huyo wa Olimpiki mara mbili alimaliza katika nafasi ya 10.

Kiplagat alishawishiwa kutojiondoa katika mbio hizo na kocha wake baada ya kifo cha mshirika wake ambaye ni mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon Kelvin Kiptum, katika ajali ya barabarani mwezi uliopita.

Soma: Kenya yaomboleza kifo cha mwanariadha Kelvin Kiptum

Upande wa wanawake mwanariadha wa Ethiopia Sutume Asefa Kebede alimaliza mbele ya bingwa mtetezi wa Kenya Rosemary Wanjiru kwa muda wa 2:15:55 na  Amane Beriso wa Ethiopia akimaliza wa tatu kwa saa  2:16:58.