Kiongozi wa zamani wa Rhodesia Ian Smith afariki dunia | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kiongozi wa zamani wa Rhodesia Ian Smith afariki dunia

Kiongozi wa zamani wa Rhodesia iliokuwa chini ya utawala wa wazungu ambayo sasa Zimbabwe Ian Smith amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88.

Hapo mwaka 1965 Smith aliongoza theluthi ya wazungu milioni moja wa Rhodesia kujitangazia uhuru kutoka kwa Uingereza kupinga mapendekezo ya utawala wa weusi walio wengi nchini humo.Aliendelea kuwa Waziri Mkuu hadi pale vita vya chini kwa chini vya wazalendo vilipomlazimisha kukubali usitishaji wa mapigano na usuluhishi wa kisiasa hapo mwaka 1979.

Uchaguzi ulifanyika mwaka uliofuatia wakati Rhodesia ilipokuwa Jamhuri ya Zimbabwe chini ya utawala wa weusi na Robert Mugabe akawa waziri mkuu.

Smith aliendelea kumpinga Mugabe hata baada ya kufutwa kwa viti vya bunge vilivyotengwa kwa wazungu hapo mwaka 1987.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com