1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Kiongozi wa Sudan aonya juu ya kuenea kwa vita

John Juma
22 Septemba 2023

Mkuu wa majeshi na kiongozi wa Sudan, jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametahadharisha kwamba vita vya nchini mwake vinaweza kuenea kwenye eneo lote la nchi zinazopakana na Sudan.

https://p.dw.com/p/4Whdh
UN-Generalversammlung | Abdel-Fattah Al-Burhan Abdelrahman Al-Burhan
Mkuu wa majeshi na kiongozi wa Sudan, jenerali Abdel Fattah al-BurhanPicha: Craig Ruttle/AP/picture alliance

Mkuu wa majeshi na kiongozi wa Sudan, jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametahadharisha kwamba vita vya nchini mwake vinaweza kuenea kwenye eneo lote la nchi zinazopakana na Sudan.

Tahadhari ya UN:Umoja wa Mataifa watahadharisha kwamba vita vya nchini Sudan vinatishia kuiteketeza nchi nzima.

Akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jenerali Burhan, amesema vita hivyo kati ya pande mbili hasimu za jeshi ni kama cheche inayoweza kuwasha moto kwenye ukanda wa nchi zinazopakana na Sudan.

Mapigano ya Sudan yashika makali kusini mwa Khartoum

Wakati huo huo Jenerali Burhan ameitaka jumuiya ya kimataifa, ikijumlishe Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kwenye orodha ya makundi ya kigaidi na kuwakabili wanaofadhili kikosi hicho walioko nje ya mipaka ya Sudan.