1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Kinyang'anyiro cha kuania madaraka Urusi

Kiini macho cha kujiuzulu waziri mkuu Fradkow na kuchaguliwa Subkow

Mada ni moja tuu na inahusu mabadiliko ya serikali mjini Moscow.Viktor Subkow-jina hili sio wengi wanalolijua,hata nchini Urusi kwenyewe.Kuteuliwa kwa mshangao wa wengi,mkuu huyo wa idara ya shughuli za fedha kua waziri mkuu badala ya Fradkow,kumewashughulisha wahariri wengi wa magazeti ya Ujerumani.Ripota wa gazeti la KÖLNISCHE RUNDSCHAU mjini Moscow amechunguza kwa makini hali ya mambo na ameandika:

“Putin ametumia mbinu zake zile zile za kawaida za hadaa kudhihirisha madaraka aliyo nayo.Akijifanya kama kiongozi aliyeshangazwa,Putin amekubali maombi ya kujiuzulu yaliyotolewa eti kwa hiari na waziri mkuu asiyekua na lake-kwasababu Fradkow kimsingi hakua na madaraka yoyote yale na kumtuza papo hapo nishani ya juu kabisa ya nchi hiyo.Mabadiliko ya serikali yanafichua kwa mara nyengine tena sura halisi ya utawala wa Putin.Kile ambacho kwengineko kinaangaliwa kama “mambo ya kiholela” mjini Moscow kinasifiwa kama ushahidi wa hali ya utulivu.”

Maoni sawa na hayo yametolewa na mhariri wa gazeti la WESTDEUTSCHE ALLGEMEINE ZEITUNG la mjini Essen:

“Kinyang’anyiro cha kuania madaraka kimeshaanza nchini Urusi-kwanza katika uchaguzi wa bunge December iliyopita,na kitaendelea baadae uchaguzi wa rais utakapoitishwa mwezi March mwakani.Rais Putin ambae kwa mujibu wa katiba inayotumika hivi sasa haruhusiwi tena kuchaguliwa kua rais,anajibwaga kwa nguvu na werevu katika uwanja aliouzowea.Ni hadaa tuu na kuwadang’anya watu wanaposema eti Putin ameukubali uamuzi wa kujiuzulu serikali yake- lengho liliwa kuonyesha eti hahusiki hata chembe na kinyang’anyiro cha kuania madaraka.”

Gazeti la LANDSHUTER ZEITUNG/STRAUBUNGER TAGBLATT linachambua:

„Rais wa Urusi ameingia mbioni kujitengenezea uwanja wa baada ya kung’atuka madarakani huko Kremlin.Kichekesho hapa sio tuu jinsi Putin alivyojitokeza pale waziri mkuu alipojiuzulu,bali matamshi aliyoyatumia. “Cha muhimu ni kubuni mkakati wa aina mpya ili kuweza kua na wakati bora kuweza kukabiliana na uchaguzi.”Kwa maneno bayana:Putin na vijana wake wa kutoka St.Petersburg wanataka kutia njiani mfumo wa kisiasa wakiwakabidhi madaraka watu wao kwa namna ambayo hakutakua na kizungumkuti na wala maajabu hayatazuka uchaguzi utakapoitishwa mwaka 2008.”

Gazeti la SÜDWEST-PRESSE la mjini Ulm linahisi kuchaguliwa Subkow kua waziri mkuu ni uamuzi wa muda tuu uliolengwa kumfikisha Kremlin ambako atakaekua na usemi huko si mwengine isipokua Putin tuu”-Gazeti linaendelea kuandika:

“Kwa muda mrefu sasa watetezi wa kiti cha rais waliokua wakipewa nafasi nzuri ya kushinda ni makamo wa waziri mkuu, Iwanov na Medwedew.Hivi sasa anachomoza mwengine wa tatu,na pengine huyo ndiye atakaechekelea-:Viktor Subkow,mkuu wa idara ya kusimamia shughuli za fedha ameteuliwa na Putin kua waziri mkuu baada ya kuwadanganya watu eti Michael Fradkow ameamua kujiuzulu.Subkow anatokea katika genge lile lile la St.Petersburg lililompandisha Putin wakati mmoja madarakani.Sasa anaweza kudhihirisha kama anaweza kupanda juu zaidi.

 • Tarehe 13.09.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHRq
 • Tarehe 13.09.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHRq