Kinu pekee cha kinuklia Afrika | Masuala ya Jamii | DW | 27.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Kinu pekee cha kinuklia Afrika

Kinu pekee cha kinuklia cha kutoa umeme barani Afrika kipo Cape Town Afrika Kusini.Afrika Kusini inapanga kujenga kinu kigne 2012.

Afrika kusini ina kinu pekee cha kinuklia cha kuzalisha nishati barani Afrika.Kipo mjini Cape Town tangu miaka 40 sasa.

Mnamo miaka michache iliopita, mara kwa mara hitilafu zikizuka katika kinu hicho.Hatahivyo, serikali ya Afrika Kusini inapanga kujenga vinu zaidi vya nishati ya kinuklia na waafrika kusini wengi, hawaoneshi kuingiwa na wasi wasi.

Kinu pekee cha kinuklia barani afrika kimekuwa kikigonga vichwa vya habari navyo si vya kupendeza.Mara kuna hitilafu katika mtambo huu mara hitilafu katika mtambo ule.Mara kwa mara kuna kasoro na kwa bahati nzuri hadi sasa hakuna ajali mbaya iliozuka isipokuwa kukosekana umeme mjini Cape Town.

“Sina tatizo kwa kadiri hakuna hatari.Bila ya shaka kumekuwapo kasoro katika kinu cha Koeberg,lakini nadhani hii inatokana na wafanyikazi wa huko.Kinu chenyewe ninavyoona hakina matatizo.”

Asema jamaa huyo.

Kinyume na wasemavyo walinzi wa sehemu ya kuegesha magari mjini Johannesberg:

”mimi sielewi chochote juu ya kinu cha nuklia.

“Nadhani kinatisha na ni hatari.Nishati ya jua ni bora kwani ni ya usalama.”

Nae mama mmoja alisema: “Nahisi nishati ya nguvu za atomiki ni ya hatari na mimi inanipa wsasi wasi.”

Mwengine akasema hajali vipi inatengezwa nishati hiyo ya kinuklia daima kuna hatari.Mtambo wa kuendeshea kinu hicho unatoa takataka za kinuklia zenye miale ya sumu ,lakini yakisafishwa sawa sawa na barabara,haoni tatizo lolote katika umeme wa kinuklia.Inategemea sana nani anaefanya kazi hapo na nani ana dhamana-aliongeza.

Raslimali katika nishati tofauti kabisa nay a vinu vya nuklia,imedharauliwa sana nchini Afrika Kusini.

Nchi hii ina upepo mwingi,jua kali na la kutosha na maji mengi.Lakini ukizungumza huko Afrika Kusini juu ya nishati ya jua,upepo au vinu vya nguvu za maji,wengi hudhani kwamba nishati za aina hiyo kwa nchi inayonyanyukia kiuchumi haifai.

Kwa kweli, nishati ya upepo na ya maji ndio mkondo mpya wa siku zijazo.Hii inawafanya baadhi kuhisi ni bora kutokua kabisa na nishati ya kinuklia.Hatahivyo, inafaa kuangalia ukweli wa mambo nao waafrika kusini ni wakaazi wengi ambao wanahitaji nishati nyingi.

Nishati mbadala haitoshi kukidhi mahitaji.Kwahivyo, nishati ya kinuklia ndio njia pekee ya kutosheleza mahitaji hayo.

Hadi sasa nishati ya nuklia ikikidhi 4% ya mahitaji yake.Sehemu iliobaki hujazwea na makaa yamawe ambayo akiba kubwa iliopo nchini yaweza kuendelea kuitosheleza hadi karne ijayo.Lakini, Afrika Kusini haiwezi kutegem,ea makaa yam awe tu na hasa kwa jicho la kuchafua mazingira.

Tangu 1994 matumizi ya umeme nchini Afrika Kusini yamepanda kutoka megawatt 20.000 kwa mwaka hadi meg.36,000.

Kinu kingine cha kinuklia ambacho kiegemee ufundi wa kizamani wa kijerumani, kimepangwa 2012 kuanza kazi.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com