KINSHASA:Mbeki afanya ziara ya kikazi Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
21 Agosti 2007Matangazo
Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini amewasili nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo kufanya ziara ya kikazi nchini humo yenye lengo la kuinua kiwango cha uhusiano baina ya nchi mbili hizo.
Rais Mbeki na wenyeji wake wanatarajiwa kutathimini ushirikiano wao katika masuala ya usalama,uchumi,fedha na katika miradi ya maendeleo.
Rais Mbeki anafanya ziara hiyo muda mfupi baada ya rais J. Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kuitembelea Afrika Kusini mnamo mwezi juni.