1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Bemba kwenda Ureno kutibiwa mguu

29 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEe

Kiongozi wa upinzani katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Jean Pierre Bemba anapanga kwenda Ureno kwa ajili ya matibabu.

Bemba amekimbilia katika ubalozi wa Afrika Kusini, mjini Kinshasa, baada ya mapigano kati ya askari wake na wale wa serikali wiki iliyopita ambapo zaidi ya watu 600 inaarifiwa waliuawa.

Ubalozi wa Afrika Kusini mjini Kinshasa,umesema kuwa Bemba amepanga kuondoka siku ya Jumamosi kwenda Ureno kutibiwa mguu.

Kiongozi anakabiliwa na mashtaka ya uhaini, lakini ana kinga ya kisiasa, ambayo serikali imesema inaagalia uwezekano wa kuiondoa ili ashtakiwe.

Serikali inamtuhumu Bemba kutaka kuipindua serikali ya Rais Joseph Kabila.

Suala hilo la hali ya kisiasa huko Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo linatarajiwa kuwa moja ya ajenda katika kikao cha leo cha dharura Mjini Dar es Salaam Tanzania cha wakuu wa nchi za SADC.