KINSHASA:Antoine Gisenga ateuliwa waziri mkuu | Habari za Ulimwengu | DW | 31.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA:Antoine Gisenga ateuliwa waziri mkuu

Kama ilivyotarajiwa na wengi huko nchini Kongo rais Joseph Kabila amemteuwa Antoine Gisenga ambaye alikuwa mpinzani ,waziri mkuu wa nchi hiyo hapo jana.

Rais Kabila pia amemtaka Gisenga kuwateuwa mawaziri wa serikali mpya.

Bwana Gisenga mwenye umri wa miaka 81 ambaye ni mwanasiasa maarufu nchini jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo kwa karibu miongo mitano alikuwa naibu waziri mkuu katika serikali iliyokuwa ikiongozwa na Patrice Lumumba.

Katika uchaguzi wa duru ya mwanzo nchini Kongo Gisenga alikuwa mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha PALU na kuambulia nafasi ya tatu akiwa na asilimia 13 ya kura.

Katika duru ya pili ya uchaguzi huo wa rais kati ya vigogo wawiwili Joseph Kabila na Jean Pierre Bemba,Gisenga alijitosa katika kumuunga mkono rais Kabila kwa sharti la kuteuliwa waziri mkuu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com