1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kinshasa. Wachimba migodi wafariki baada ya kuporomoka.

Kiasi wachimba migodi saba wamefariki wakati machimbo ya Almasi yalipoporomoka katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo jana. Radio ya umoja wa mataifa ya Okapi imewanukuu polisi wakisema kuwa miili saba ya wachimba migodi hao i mepatikana lakini watu walioshuhudia wamesema kuwa watu kadha walikuwa chini ya ardhi wakati machimbo hayo yalipoporomoka usiku wa kuamkia Jumanne.

Gavana wa jimbo la Kasai Alphonse Ngoy Kasanji ameliambia shirika la habari la AFP kuwa watu kadha ambao wanafanyakazi kinyume na sheria katika migodi hiyo wako bado ndani ya mgodi huo na ni vigumu kufahamu ni wangapi bado wako chini ya ardhi wakati ajali hiyo inatokea.

Wakati huo huo waasi wa Kihutu kutoka Rwanda wameongeza mashambulizi yao mashariki ya jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, wakiuwa watu watatu na kuwakamata watu wengine kadha katika siku za hivi karibuni, ujumbe wa umoja wa mataifa umesema jana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com