KINSHASA : Vikosi hasimu vyajiandaa kwa mapambano | Habari za Ulimwengu | DW | 01.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA : Vikosi hasimu vyajiandaa kwa mapambano

Wanajeshi wa kawaida katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,vikosi vilivyoasi na waasi wa Rwanda wamekuwa wakijiandaa kwa mapigano zaidi hapo jana.

Msemaji wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa MONUC Sylvie van den Wildenberg amesema usiku kwa jumla ulikuwa shwari katika jimbo la Kivu ya Kaskazini baada ya mapigano makali kati ya jeshi na waasi wa generali Laurent Nkunda hapo Alhamisi.

Helikopta za kivita za MONUC zimekuwa zikiruka kwenye jimbo hilo usiku kucha kutokana na kuonekana nyendo za kijeshi kwenye mpaka wa jimbo hilo na Rwanda.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com